Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

TAASISI YA USULUHISHI WA MALALAMIKO NA TAARIFA ZA KODI

"Haki na Usawa"

Types of complaints

Ofisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi (TOST) inapokea na kushughulikia aina za malalamiko zifuatazo:

1. Malalamiko ya Huduma

Haya ni malalamiko yanayohusu kutokuzingatiwa kwa viwango vya utoaji huduma vilivyowekwa katika Mkataba wa Huduma kwa Mteja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Malalamiko haya yanaweza kujumuisha kushindwa kutoa huduma kwa wakati, kutoshughulikia maswali au malalamiko ya walipakodi ipasavyo, pamoja na ukiukwaji mwingine wa viwango vya huduma.

2. Malalamiko ya Kiutaratibu

Haya ni malalamiko yanayotokana na kutokufuatwa kwa taratibu za kiutendaji zilizowekwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ikiwemo Taratibu za Ubora wa Utoaji Huduma (Quality Service Procedures - QSP) na taratibu nyingine zinazotumika katika usimamizi wa kodi.

3. Malalamiko ya Kiutawala

Haya ni malalamiko yanayohusiana na dosari au kasoro katika utekelezaji wa sheria za kodi au utawala wa kodi, ikiwa ni pamoja na matumizi yasiyo sahihi ya mamlaka, ucheleweshaji usio wa lazima, kutofuata kanuni au taratibu za kiutawala, pamoja na vitendo vingine vinavyoweza kusababisha kutotendewa haki kwa mlipakodi.