Historia
Ofisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi (TOST) ilianzishwa kufuatia marekebisho ya Sheria ya Usimamizi wa Kodi, Sura ya 438, yaliyopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwezi Juni 2019 na kuanza kutumika rasmi mwezi Julai 2019. Hata hivyo, ofisi ilianza kutekeleza majukumu yake rasmi mwezi Januari 2024.
Lengo kuu la Ofisi ya TOST ni kulinda haki za walipakodi kwa kutoa huduma ya usuluhishi wa malalamiko ya kodi kwa haki na usawa. Ofisi hii ni chombo huru chenye jukumu la kupokea, kupitia, kuchunguza na kushughulikia malalamiko yanayowasilishwa na mtu yeyote kuhusu huduma, taratibu au masuala ya kiutawala yanayojitokeza katika utekelezaji wa Sheria za Usimamizi wa Kodi unaofanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Kamishna Mkuu au watumishi wa Mamlaka hiyo.