Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

TAASISI YA USULUHISHI WA MALALAMIKO NA TAARIFA ZA KODI

"Haki na Usawa"

Wajibu

Kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi wa Kodi, Sura ya 438, Ofisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi ina mamlaka ya kupitia, kuchunguza na kushughulikia malalamiko yoyote yanayowasilishwa na mtu yeyote kuhusu huduma, taratibu au masuala ya kiutawala yanayotokana na utekelezaji wa sheria za kodi unaofanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).