Misingi Mikuu
Utekelezaji wa Majukumu ya Ofisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi unaongozwa na maadili ya msingi matano (5) yanayoelekeza mwenendo wa ndani wa Ofisi pamoja na mahusiano yake na wadau.
Uadilifu
Tunazingatia uzalendo, maadili mema, uaminifu, uwajibikaji, nidhamu, utii wa sheria, uwazi na dhamira ya utekelezaji wa majukumu. Tunahakikisha kuwa watumishi wanatoa huduma kwa heshima, unyenyekevu na weledi kwa manufaa ya umma.
Weledi
Tunazingatia viwango vya juu vya taaluma, ujuzi, umahiri na uzoefu katika utekelezaji wa majukumu ya kila mtumishi. Pia tunahamasisha kujifunza, matumizi ya teknolojia, fikra bunifu na kufanya maamuzi sahihi kwa wakati.
Uhuru
Tunafanya kazi kwa uhuru katika kutekeleza majukumu bila kuathiriwa na maslahi binafsi, shinikizo au ushawishi usiofaa, ili kuhakikisha haki inatendeka.
Usawa
Tunatoa huduma kwa haki, bila upendeleo na kwa kuzingatia usawa kwa wadau wote tunaowahudumia.
Usiri
Tunazingatia kiwango cha juu cha usiri na kulinda taarifa zote tunazozipata wakati wa kutekeleza majukumu yetu, kwa mujibu wa sheria na maadili ya utumishi wa umma.