TOST JIPANGE VIZURI KUWASAIDIA WANA DAR ES SALAAM

Ofisi ya Msuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi wekeni mikakati mizuri ya kutoa elimu kwa Wananchi na walipa kodi kwa ajili ya manufaa ya Taifa letu ili kusaidi kutatua malalamiko ya kikodi kwa lengo la kuongeza ulipaji kodi kwa hiari kwa wananchi na wafanyabiashara.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila ameyasema hayo katika Uzinduzi wa Kampeni ya Elimu kwa Umma inayoendelea Viwanja vya Mnazi Mmoja na kuisisitiza Ofisi hiyo indelee kusimamia na kuboresha utendaji wake kwa kuhakikisha mahaitaji yote ya muhimu yanapatikana ikiwemo vifaa na mifumo ya kisasa ili iweze kutoa huduma za kisasa kwa wananchi na walipakodi wote nchini.
Niwaombe sana msipuuze malalamiko kwasababu Biashara ni kitu ambacho kinabadirikabadirika (Kupanda au kushuka) tuhakikishe mifumo ya ulipaji kodi inaendana na panda shuka zinazojitokeza kwenye biashara ili lengo kupunguza migogoro ya kikodi.
Kwahiyo niwasii Watanzania wote na hasa wanaDSM kujitokeza kwa wingi kama wadau wakubwa wa ofisi hii ya Msuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi mpaka kilele chake ifikapo Juni 27, matumaini yangu kuwa ofisi hii imejiandaa kwa kuja na mikakati mizuri ya usuluhishi itakayopelekea Mfanyabiashara na serikali kuonwa kama ni ndugu na siyo adui tena ili kuongeza tija katika ukusanyaji wa mapato.