Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

TAASISI YA USULUHISHI WA MALALAMIKO NA TAARIFA ZA KODI

"Haki na Usawa"

KAMPENI YA KUTOA ELIMU PAMOJA NA KUPOKEA MALALAMIKO NA TAARIFA ZA KODI KATIKA MKOA WA DAR ES SALAAM

Imewekwa: 21 Jun, 2024
KAMPENI YA KUTOA ELIMU PAMOJA NA KUPOKEA MALALAMIKO NA TAARIFA ZA KODI KATIKA MKOA WA DAR ES SALAAM

Tunafahamu mkoa wa Dar es Salaam kuna mchango mkubwa sana wa kodi kutokana na kuwa lango kuu la biashara , kwahiyo kama Ofisi imekuwa ni jambo la muhimu kwetu kuwaletea huduma hii muhimu kwa kufika Mkoa huu.

Kulingana na umuhimu huo ofisi ya Msuluhushi imeandaa kampeni hii maalum ili wanachi wapete Elimu itakayowawezesha kuifahamu ofisi hii, kufahamu wajibu na majukumu ya ofisi hii, kufahamu namna ya kuwasilisha malalamiko waliyonayo kwenye masuala ya kodi na kufahamu pia faida za kutumia huduma hii. Hayo yamesemwa na Msuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi Bw. Erastus V. Mtui siku uzindizu wa kampeni ya siku 9 katika Mkoa wa Dar es salaam

Msuluhishi ametoa wito kwa wananchi wawe huru kuitumia ofisi hii kwakuwa chombo hiki kimeundwa na Serikali ya Awamu ya sita chini ya Rais DKT. SAMIA SULUHUS HASSAN kwa lengo la kuwasaidia walipakodi na wananchi kwa ujumla.