Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

TAASISI YA USULUHISHI WA MALALAMIKO NA TAARIFA ZA KODI

"Haki na Usawa"

How to lodge complaints

Mlipakodi au mwananchi yeyote anaweza kuwasilisha malalamiko ya kodi au taarifa za kodi kwa Ofisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi (TOST) kupitia njia zifuatazo:

  • Kutembelea Ofisi za TOST

Tembelea ofisi ya TOST iliyopo jengo dogo la Hazina Mji wa Serikali – Mtumba, Dodoma au Hazina ndogo Dar es Salaam uwasilishe malalamiko yako kwa maandishi au kwa maelezo ya mdomo kwa afisa anayehusika.

 

  • Kuwasilisha kwa Njia ya Posta

Tuma malalamiko yako ya kodi pamoja na nyaraka zote za uthibitisho kupitia anuani ifuatayo: Ofisi ya Usuluhishi wa Ma//lalamiko na Taarifa za Kodi (TOST)

S.L.P. 1441, Mji wa Serikali – Mtumba, Dodoma, Tanzania.

 

  • Kuwasilisha kwa Barua Pepe

Tuma malalamiko au taarifa zako za kodi kupitia mojawapo ya barua pepe zifuatazo: malalamiko@tos.go.tz, service@tos.go.tz au huduma@tos.go.tz

 

  • Kupiga simu bila malipo (Kituo cha Huduma kwa Wateja)

Piga simu bila malipo kupitia namba: 0800 111 022, Huduma hii inapatikana siku za kazi, Jumatatu hadi Ijumaa, kuanzia saa 2:30 asubuhi hadi saa 10:00 jioni.

 

  • Mfumo wa Kusimamia Malalamiko ya Kodi (TCMS)

Wasilisha malalamiko yako kwa njia ya mtandao kupitia Mfumo wa Kusimamia Malalamiko ya Kodi (TCMS) unaopatikana kupitia tovuti ya TOST: www.tos.go.tz au moja kwa moja kupitia kiungo: https://tcms.tos.go.tz/tos

 

  • Programu ya Simu ya Suluhu ya Kodi

Wasilisha malalamiko yako kwa urahisi kupitia Programu ya Suluhu ya Kodi (SuluhuyaKodi App) inayopatikana kwenye simu za Android (Playstore) na iPhone (iOS).

 

  • WhatsApp

Wasilisha malalamiko au taarifa za kodi kupitia namba rasmi ya WhatsApp:

+255 736 010 022

 

  • Kupiga *152*00#

Kisha utachagua namba 10 Mbele,

Kwenye huduma za Serikali chagua namba 6 (Suluhu ya Kodi) kupata huduma zote za TOST ikiwemo Tuma Lalamiko, Toa Taarifa, Fuatilia Lalamiko/Taarifa, Msaada