Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

TAASISI YA USULUHISHI WA MALALAMIKO NA TAARIFA ZA KODI

"Haki na Usawa"

WANANCHI ITUMIENI TOST KUTATUA CHANGAMOTO ZENU ZA KODI

Imewekwa: 07 Jun, 2024
WANANCHI ITUMIENI TOST KUTATUA CHANGAMOTO ZENU ZA KODI

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule ametoa rai hiyo kwa wafanyabiashara na wananchi kuitumia Ofisi ya Msuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi (TOST) katika kushughulikia maalalamiko ya Kodi waliyonayo.

Mhe. Senyamule amesema kufanya hivyo kutaisaidia Serikali kuboresha huduma za ulipaji kodi pamoja na kutatua changamoto zote zinazohusu usimamizi wa sheria za kodi kama ilivyo dhamira ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DKT. SAMIA SULUHU HASSAN anavyo sisitiza wajibu wa kulipa kodi na kukemea dhuluma wakati wa kukusanya kodi hizo.

Aidha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma amewaagiza watendaji wa Ofisi ya Msuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za kodi kutoa Elimu kwa umma juu ya majukumu yanayotekelezwa na ofisi hii na kuzingatia weledi katika kushughulikia changamoto zinazowasilishwa kwao kutoka kwa Wafanyabiashara na Wananchi kwa haki na usawa. Kwa kufanya hivyo mtakuwa mmetimiza lengo la kuundwa kwa Ofisi hiyo na hivyo ulipaji wa kodi kwa kila mtanzania itakuwa ni tabia ya hiari na siyo shuruti tena.

Hayo yameelezwa wakati wa Ufunguzi wa Kampeni ya Elimu kwa Umma Jijini Dodoma iliyofanyika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na baadaye Kampeni hiyo kuanza utekelezwaji wake katika Viwanja vya Nyerere Square kwa kuwahudumia Wananchi na Wafanyabiashara.