Sera ya Faragha
SERA YA FARAGHA YA PROGRAMU YA SIMU – (SuluhuyaKodi)
Sera hii ya Faragha inaeleza jinsi Programu ya Simu ya SuluhuyaKodi inavyokusanya na kulinda taarifa zako binafsi unazotupatia, au zinazopatikana/kuzalishwa wakati unapopakua, kufikia, au kutumia huduma zetu.
1. Taarifa Tunazokusanya
Programu ya SuluhuyaKodi hupokea au hukusanya taarifa wakati tunapotoa huduma zetu, ikiwa ni pamoja na wakati wa usakinishaji, usajili, na matumizi ya kawaida ya programu.
a) Taarifa Unazotoa
-
Taarifa za Akaunti: Unatupatia namba yako halali ya simu ya mkononi, anwani ya barua pepe, jina kamili, Namba ya Utambulisho wa Mlipa Kodi (TIN), na taarifa nyingine zinazohusiana na kodi ili kuunda na kusimamia akaunti yako.
-
Msaada kwa Wateja: Unapowasiliana nasi (kwa barua pepe, simu, au kupitia programu), unaweza kutoa taarifa kuhusu matatizo unayokutana nayo, utendaji wa programu, au maoni yako.
b) Taarifa Zinazokusanywa Moja kwa Moja
-
Taarifa za Matumizi na Rekodi: Tunakusanya taarifa za uchunguzi na utendaji wa huduma, kama vile jinsi unavyotumia programu, faili za rekodi, na ripoti za uchunguzi au utendaji.
-
Taarifa za Kifaa: Tunaweza kukusanya maelezo ya kifaa chako kama vile aina ya kifaa, toleo la mfumo wa uendeshaji, toleo la programu, na taarifa za mtandao wa simu.
2. Jinsi Tunavyotumia Taarifa
Tunatumia taarifa tunazokusanya ili kuendesha, kuboresha, na kulinda Programu ya SuluhuyaKodi, ikiwa ni pamoja na:
-
Kutoa Huduma: Ili kuwezesha usajili, uwasilishaji wa taarifa za kodi, na huduma nyingine za kikodi kupitia programu.
-
Huduma kwa Wateja: Kujibu maswali, kutatua matatizo, na kuboresha uzoefu wa mtumiaji.
-
Kuboresha Huduma: Kuchambua mwenendo wa matumizi na kukusanya takwimu ili kuboresha utendaji wa programu.
-
Usalama na Ulinzi: Kuthibitisha akaunti na shughuli za watumiaji, kuchunguza shughuli za kutiliwa shaka, kuhakikisha uzingatiaji wa sheria, na matumizi halali ya programu.
3. Ulinzi wa Taarifa
Tumejikita katika kuhakikisha taarifa zako zinalindwa. Tunatekeleza hatua stahiki za kiufundi na kiutawala kuzuia ufikiaji, ufichuaji, mabadiliko, au uharibifu wa taarifa zako binafsi bila idhini.
4. Mabadiliko ya Sera ya Faragha
Tunaweza kusasisha Sera hii ya Faragha mara kwa mara ili kuendana na mabadiliko ya kiteknolojia, sheria, au huduma zetu. Mabadiliko yoyote yatachapishwa ndani ya Programu ya SuluhuyaKodi na kwenye tovuti yetu rasmi: https://www.tos.go.tz
5. Wasiliana Nasi
Ikiwa una maswali au wasiwasi wowote kuhusu Sera hii ya Faragha au taarifa zako binafsi, tafadhali wasiliana nasi kwa:
Huduma ya Usuluhishi wa Malalamiko ya Kodi (TOS)
Simu: 0800111022
Barua Pepe: service@tos.go.tz
Tovuti: https://www.tos.go.tz
Anuani ya Posta: TAASISI YA USULUHISHI WA MALALAMIKO NA TAARIFA ZA KODI, S.L.P 1441, DODOMA, Tanzania.