TCCIA YAKOSHWA NA HUDUMA ZA TOST KATIKA MAONESHO YA 20 YA BIASHARA AFRIKA MASHARIKI

Uongozi wa Chemba ya Wafanyabiashara, Wenye Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) umefurahishwa na huduma zinazotoelewa na Ofisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi (TOST) katika Maonesho ya 20 ya Biashara Afrika Mashariki yanayofanyika Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza. Wakizungumza na Maafisa wa TOST Makamu wa Rais Biashara TCCIA - BONIFACE NDENGO na Makamu wa Rais Viwanda TCCIA - ABDUL MWILIMA wameomba kupewa Elimu ili wawe na ujuzi wa kuwasaidia Wawekezaji watakapopata changamoto kwenye maswala ya Kodi.
Kwa upande wake WITTNES MOLLEL Kaimu Meneja wa Usajili Malalamiko amesema TOST ipo tayari kushirikiana na Chemba ya Wafanyabiashara, Wenye Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) ili kuleta tija kwenye sekta ya Uwekezaji ili kupunguza malalmiko ya Kodi yatakayopelekea kuongezeka kwa Mapato.