TUNAITEGEMEA TOST ILETE URAFIKI NA UHALALI KWENYE UKUSANYWAJI WA KODI

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mhe. Jabir Shekimweri ameimbia Ofisi ya Msuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi (TOST) kuna haja ya kuangalia mfumo mzima wa utaratibu wa zoezi la ukusanywaji wa kodi kuzingatia kiwango, muda na mahali.
Ofisi ya msuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi (TOST) mkisimamia hayo kwa uweledi ni dhahiri shahiri mtakuwa mmejenga urafiki baina ya mlipa kodi na Mamlaka ya Mapato ili kuwasaidia walipa kodi kulipa kodi kwa hiyari bila kutumia nguvu wala mabavu.
Kwa kufanya hivyo ni wazi mtakuwa mmeleta suluhu kwa wananchi na kutimiza azima ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DKT. SAMIA SULUHU HASSAN ya kuunda ofisi hii ili kuleta tija na kuondosha tabia ya ukwepaji wa kodi bila kusahau kuondosha kodi za dhuluma kwa maendeleo ya Taifa letu.
Mhe. Shekimweri amayesema hayo kwanye hafla ya uzinduzi wa Kampeni ya Elimu kwa Umma iliyofanyika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Dodoma yenye kauli mbiu ya Kataa ukwepaji kodi, Kataa kodi za Dhuluma.