Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

TAASISI YA USULUHISHI WA MALALAMIKO NA TAARIFA ZA KODI

"Haki na Usawa"

TOST NI MSULUHISHI WA BURE WA MALALAMIKO YOTE YA KODI ZINAZOSIMAMIWA NA TRA

Imewekwa: 07 Jun, 2024
TOST NI MSULUHISHI WA BURE WA MALALAMIKO YOTE YA KODI ZINAZOSIMAMIWA NA TRA

Ofisi ya Msuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi (TOST) inatekeleza majuku yake kwa Uhuru bila kusimamiwa wala kufungamana au kupendelea upande wowote, inazingatia weledi na uadilifu, inatenda kwa haki na usawa, inatunza siri. Hivyo mfanyabiashara au mwananchi yeyote mwenye malalamiko ya Kodi au Taarifa za Kodi kuleta TOST kusudi tuyafanyie kazi.

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Elimu kwa Umma Bw. Edwin Iwato amasema TOST inashughulikia malalamiko yote ya Kodi zinazosimamiwa na TRA, aina hizo za malalamiko zimegawanyika katika maeneo matatu ambayo ni maeneo ya utohaji wa huduma, utaratibu unasimamiwa na TRA pamoja na usimamizi wa sheria na kanuni za kodi unavyotekelezwa na TRA.

Bw. Iwato ameeleza kuwa malalamiko hutokea kutokana na kuenenda kinyume na taratibu zinazokubalika katika utoaji wa huduma, utendaji usiofuata taratibu na maamuzi yasiyofuata Sheria za Usimamizi wa kodi. Serikali imeunda ofisi ya Msuluhishi wa malalamiko na Taarifa za Kodi ila kuleta suluhu na upatanishi kati ya Mlipa Kodi na TRA. Na kusisitiza kuwa huduma hiyo ya kupokea na kuchakata malalamiko inatolewa bure bila malipo yoyote kwa Msuluhishi. 

Hayo ameyasema mkuu wa kitengo cha Habari na Elimu kwa Umma Bw. Edwin Iwato kutoka Ofisi ya Msuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi alipokuwa akishiriki kipindi cha JAMVI cha TBC Dodoma Radio Jamii.