KARIBU KATIKA BANDA LA OFISI YA USULUHISHI WA MALALAMIKO NA TAARIFA ZA KODI (TOST)
Ofisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi (TOST) inakukaribisha kutembelea banda lake katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) 2026, yanayofanyika katika Viwanja vya Mwl. Julius Kambarage Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Tembelea banda letu upate huduma mbalimbali bila malipo, ikiwemo:
• Ushauri kuhusu masuala ya kodi.
• Kupokea na kushughulikia malalamiko ya kodi kwa ajili ya usuluhishi.
• Elimu ya kodi ili kuongeza uelewa kuhusu sheria na taratibu za kodi.
• Ufafanuzi kuhusu haki na wajibu wako kama mlipakodi, pamoja na mwongozo sahihi wa masuala ya kodi.
Banda la TOST linapatikana ndani ya Jengo la Wizara ya Fedha.
Tunawakaribisha wananchi wote, wafanyabiashara na wadau mbalimbali kutembelea banda letu na kupata huduma kwa haraka, weledi na bila gharama yoyote.
Mlalamikaji au mtoa taarifa anaweza kuwasilisha malalamiko au taarifa za kodi kupitia njia zifuatazo:
• Simu ya bure: 0800 111 022
• WhatsApp: 0736 010 022
• Barua pepe: service@tos.go.tz
• Aplikesheni ya Suluhu ya Kodi
• Mfumo wa TCMS: https://tcms.tos.go.tz/tos (unapatikana pia kupitia tovuti ya www.tos.go.tz)
• Sanduku la Posta: SLP 1441, Dodoma
• Kutembelea ofisi za TOST, zilizopo Hazina Ndogo, Dar es Salaam, na Jengo la Wizara ya Fedha, Mji wa Serikali – Mtumba, Dodoma.
@tostanzania inahakikisha usiri wa taarifa za mlalamikaji au mtoa taarifa kwa mujibu wa sheria.