TOST YAPONGEZWA KWA MAGEUZI YA KIDIJITALI KATIKA USULUHISHI WA MALALAMIKO YA KODI
TOST YAPONGEZWA KWA MAGEUZI YA KIDIJITALI KATIKA USULUHISHI WA MALALAMIKO YA KODI
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Luswetula, ameipongeza Ofisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi (TOST) kwa matumizi ya teknolojia katika kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi wenye malalamiko na taarifa za kodi, bila kulazimika kufika ofisini.
Akitembelea banda la TOST katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), Mhe. Luswetula aliitaka taasisi hiyo kuendelea kubuni, kuimarisha na kuboresha mifumo ya kidijitali ili kuongeza ufanisi na upatikanaji wa huduma kwa wananchi.
Kwa upande wake, Afisa Sheria Mkuu wa TOST, Aderickson Njunwa, amesema kwa sasa TOST inapokea na kushughulikia malalamiko na taarifa za kodi kupitia Mfumo wa Tax Complaints Management System (TCMS), Aplikesheni ya Suluhu ya Kodi, barua pepe service@tost.go.tz, simu ya bure 0800 111 022, WhatsApp 0736 010 022, pamoja na anuani ya posta S.L.P. 1441, Dodoma.
Ameeleza kuwa matumizi ya njia hizo mbalimbali ni sehemu ya jitihada za TOST kwenda sambamba na maendeleo ya teknolojia, kurahisisha wananchi kupata huduma kwa haraka na kwa urahisi, bila kuathiri shughuli zao za kila siku za kiuchumi.