Matukio katika picha kutoka Tanzania Ombudsman Forum 2026, uliofanyika tarehe 7–8 Septemba 2026 katika Hoteli ya Gran Meliá, jijini Arusha.
Matukio katika picha kutoka Tanzania Ombudsman Forum 2026, uliofanyika tarehe 7–8 Septemba 2026 katika Hoteli ya Gran Meliá, jijini Arusha.
Ofisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi (TOST) iliandaa mkutano wa masuala ya usuluhishi (Tanzania Ombudsman Forum 2026), Mkutano huo uliofanyika tarehe 7–8 Septemba 2026 katika Hoteli ya Gran Meliá, jijini Arusha. Mkutano huo uliwakutanisha zaidi ya washiriki 380 kutoka sekta mbalimbali, zikiwemo huduma za jamii, kodi, benki, bima na biashara.
Mkutano huo uliwakutanisha pia wadau kutoka zaidi ya nchi tisa, zikiwemo Kenya, Uganda, Nigeria, Botswana, Afrika Kusini, Pakistan na Australia, kwa lengo la kubadilishana uzoefu, maarifa na mbinu bora katika masuala ya usuluhishi na utatuzi wa migogoro.
Kupitia mkutano huo, TOST iliweza kuongeza uelewa kuhusu dhana, umuhimu na nafasi ya usuluhishi katika kutatua migogoro, hususan kwa wananchi, wafanyabiashara na wawekezaji. Aidha, mkutano huo ulitoa fursa kwa wadau kujadili uzoefu na mbinu mbalimbali zinazoweza kuimarisha mifumo ya usuluhishi na kuchangia katika kujenga mazingira rafiki ya biashara na uwekezaji nchini Tanzania.